Watahiniwa 566,840 kuanza mtihani Kidato cha Nne kesho

NA DAIRAMAKINI

LEO Novemba 13, 2022 Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema jumla ya watahiniwa 566,840 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, utakaoanza kesho Novemba 14, 2022 katika shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Athumani Amasi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, mtihani huo utafanyika katika jumla ya shule 5,212 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,794 nchini kote.

Pia amesema kati ya watahiniwa 566,840 waliosajiwa kufanya mtihani huo watahiniwa wa shule ni 535,001 na watahiniwa wa kujitegemea ni 31,839.

Amasi amefafanua kuwa, kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 247,131sawa na asilimia 46.19 na wasichana ni 287,870 sawa na asilimia 53.81 huku wenye mahitaji maalumu wakiwa 852.

Katika hatua nyingine amesema, maandalizi yote kwa ajili ya kufanyika mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani na vijitabu vya kujibia mitihani hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news