WAZIRI DKT.MABULA AKUTANA NA MEYA WA JIJI LA BUSAN KOREA KUSINI

NA MWANDISHI WETU 

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe. Dkt.Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Busan Metropolitan nchini Korea Kusini, Mhe. Park Heong-Joon.

Katika mazungumzo yao yaliyofamyika Novemba 3, 2022, Meya wa jiji hilo ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini baada ya Seoul alionesha nia ya kuendeleza mahusiano baina ya nchi hizo mbili yaliyodumu kwa takribani miaka 30 sasa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt.Angeline Mabula (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Meya wa Jiji la Busan Korea Kusini, Mhe. Park Heong-Joon Novemba 3, 2022 wakati wa ziara yake nchini humo.

Aidha, Mhe. Park Heong- Joon alionesha nia ya jiji lake kuwa na program za kubadilishana uzoefu kwenye nyanja za elimu sambamba na kuwa tayari kusaidia masuala ya miundombinu.

Pia Meya huyo wa Jiji la Busan Korea Kusini alionesha nia ya kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara mapema mwakani.

Waziri wa Ardhi Dkt. Mabula yuko katika ziara nchini Korea Kusini ambapo mbali na mambo mengine anashiriki mijadala kwenye maonesho ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa za kijiografia - Smart Geospatial Expo 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula (kushoto) akimkabidhi zawadi Meya wa Jiji la Busan Korea Kusini Mhe. Park Heong-Joon Novemba 3, 2022 wakati wa ziara yake nchini humo.

Mwanzoni mwa ziara yake nchini Korea Kusini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula na yule wa Ardhi Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini Bw. Won Hee-ryong walisaini makubaliano ya ushirikiano wa kuimarisha sekta ya ardhi kupitia hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news