Waziri Dkt.Tax ateta na Balozi wa Urusi na Iran nchini

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax leo tarehe 23 Novemba 2022 kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo mbali na kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia, vilevile yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa pande zote mbili na kimataifa ikiwemo biashara na uwekezaji, utalii, amani na usalama na kuendeleza sekta ya uvuvi na kilimo nchini.

Dkt. Tax akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan ameeleza kuwa licha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia uliopo kati ya mataifa haya mawili, Urusi imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini. Hivyo serikali itaendelea kudumisha na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na kuangalia maeno mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.

Kwa upande wake Balozi wa Irani nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza na Waziri Dkt. Tax ameeleza kuwa Iran inaingalia Tanzania kama mbia muhimu wa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku akielezea nia ya Iran ya kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, uvuvi na uendelezaji wa makazi.

Aidha Waziri Dkt. Tax ameeleza utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. 

Alieleza kuwa juhudi hizo zinahusisha hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanya maboresho ya kanuni, sera na sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya bishara na uwekezaji nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma.

Kwa upande wake Balozi wa Irani nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza na Waziri Dkt. Tax ameeleza kuwa Iran inaingalia Tanzania kama mbia muhimu wa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku akielezea nia ya Iran ya kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, uvuvi na uendelezaji wa makazi.

Aidha Waziri Dkt. Tax ameeleza utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Alieleza kuwa juhudi hizo zinahusisha hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanya maboresho ya kanuni, sera na sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya bishara na uwekezaji nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news