NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Nishati, January Makamba amehitimisha Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ambapo pamoja na mambo mengine amesema,mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (National Gas Neutralisation Master Plan) ambao utafanya utafiti kuhusu gesi asilia utatoa majawabu.
"Kumekuwa na maneno mengi kuhusu gesi ya Mtwara, wengine wanauliza mbona haionekani?, mbona haifiki majumbani?, huu mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (National Gas Neutralisation Master Plan) ambao utafanya utafiti kuhusu gesi asilia ndio utatoa majawabu.
“Hii itaweka mazingira ya uwekezaji katika kusambaza gesi majumbani na sekta binafsi, mazingira ya kutenga gesi Kwa kila matumizi, hii tutafanya, pesa tunayo na kazi hii itaisha ndani ya miezi mitatu.
“Kuhusu mfuko wa nishati safi ya Kupikia hapa nchini sio jambo dogo na Kiongozi wa nchi alielekeza sisi ndio tunakwenda chini kuchambua, tangu jana yale maagizo yalivyotoka kichwani kwangu yalikuwa mambo manne factions, mandate, structure na finance ya mfuko, je uanzishwe kisheria?, tutatoa mapendekezo yetu mapema sana ili mambo yakiwa mazuri mfuko uwe operational,"amesisitiza.