
Miili
ya marehemu waliofariki katika ajali ya ndege ya Shirika la Precision
iliyotokea Novemba 6, 2022, ikiwa imewekwa katika eneo maalum kwenye
uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa na
kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu katika maombolezo yaliyofanyika kweye
uwaja huo Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza na kumfariji kijana Jackson Majaliwa
kwa ushujaa wake wa kuwahi katika eneo ilipotokea ajali ya ndege ya
Shirika la Precision na kuwaokoa abiria waliokuwa wameshindwa kutoka
ndani ya ndege hiyo. Maombolezo ya kuaga miili ya watu wa ajali hiyo
yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera
7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).