NA DIRAMAKINI
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewajulisha wananchi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (SURA ya 113) kifungu cha 44 kila mmiliki wa ardhi anatakiwa kutimiza masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na sharti la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Novemba 18, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi.
Pia ameeleza kuwa, baadhi ya wamiliki wamevunja sharti hilo kwa mujibu wa kifungu cha 45 la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka.
"Hivyo, natoa taarifa kwamba, wananchi wote wanaodaiwa kodi ya pango la ardhi wanapewa nafasi ya mwisho kulipa kodi ya pango ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya tangazo hili (Novemba 18, 2022). Baada ya muda huu kupita taratibu za kisheria za ubatilisho wa miliki zitaendelea,"amefafanua Dkt.Kijazi kupitia taarifa hiyo.