NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuimarisha utendaji Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatoa mafunzo kwa viongozi na watumishi juu ya masuala ya itifaki kwa lengo la kuwajengea uwezo.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMjxNpKrYci2d-7QlDRlkZCOtQknQq8UQPeZDlryFOecAwI9hCqluM8RpJupF1yedA5BcdROtX9RQaqVliw85LeXRkmJ9m8XBpaMMjyKUUn5-xqNJJ4fHmobvrpMzgnC6ZHJFgTdOMWjRhxXWiDRkdwFsKgBdczdO7KERvP_-9nIDv1Kr38ESQKWr-Lg/s16000/IMG-20221101-WA0038.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMjxNpKrYci2d-7QlDRlkZCOtQknQq8UQPeZDlryFOecAwI9hCqluM8RpJupF1yedA5BcdROtX9RQaqVliw85LeXRkmJ9m8XBpaMMjyKUUn5-xqNJJ4fHmobvrpMzgnC6ZHJFgTdOMWjRhxXWiDRkdwFsKgBdczdO7KERvP_-9nIDv1Kr38ESQKWr-Lg/s16000/IMG-20221101-WA0038.jpg)
Akifungua mafunzo hayo jijini Dodoma Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Francis Michael amewataka viongozi na watumishi hao kuhakiksha wanashiriki kikamilifu ili matokeo ya mafunzo hayo yaweze kuonekana katika utendaji.
"Nimezisikia mada ambazo mtakwenda kufundishwa zote ni muhimu na zina tija katika kuimarisha utendaji na utoaji huduma kwa wateja ndani na nje ya wizara, hakikisheni mnashiriki kikamilifu,"amesema Dkt. Michael.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhyEmQRz_uUkT6HMNmpyutGJ_JFiyxmcPIQ_ntYm8JJILWVRpn_bsedxkb8hX58Oq8Y_inFfoSKQDGr2ZwV49D2xeu63JMl4L-eKHjchXI1yioTRC_gEMSLLP50GVU5jgI0rPBICU6zzyXVU29F1rW_sN8rzDcnGw1nnEgJ6Irs-UNefdyTiejS9rqAVg/s16000/IMG-20221101-WA0040.jpg)