NA DIRAMAKINI
JESHI la Polisi Tanzania kupitia Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Anti Drugs Unit) kwa kushirikiana na polisi mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa dawa za kulevya pamoja na vifaa mbalimbali.
Mkuu wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP AMON KAKWALE amesema kuwa,kuanzia mwezi Julai hadi Novemba, 2022, jumla ya kesi 369 zilifikishwa mahakamani na kutolewa uamuzi.
Amebainisha kuwa, jumla ya watuhumiwa 377 walitiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya.Pia amesema watuhumiwa 170 walifungwa vifungo mbalimbali kwa makosa hayo.
ACP Kakwale ameongeza kuwa, vyombo vya moto vilivyokamatwa na kutaifishwa ni magari nane, pikipiki tisa, boti mbili na nyumba moja vilitaifishwa na Mahakama kuwa mali za Serikali.
Tags
Habari
Jeshi la Polisi Tanzania
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)