Afa kwa shoti ya umeme akiweka mti wa Krismasi wa chuma nchini Guyama

NA DIRAMAKINI

PENGINE huenda ukawa ni mwanzo wa kusikitisha wa Msimu wa Krismasi kwa familia huko nchini Guyana, kwani mwanaume wa miaka 29 wa Kijiji cha Good Hope amekufa baada ya kupigwa shoti na umeme alipokuwa akiweka mti wa Krismasi wa futi 27 huko Lusignan.

Mti wa Krismasi wa chuma ambao uliguswa na waya huko Guyana na kusababisha maafa kwa wahusika. (Picha na Jeshi la Polisi Guyana).

Marehemu ametambuliwa kwa jina la Deepak Ramdeen, ambaye ni mbobezi katika masuala hayo ya mapambo huko Good Hope Mashariki ya Pwani ya Demerara.

Guyana ni nchi iliyopo kwenye Pwani ya Atlantiki ya Kaskazini ya Amerika Kusini ambapo mji mkuu wake ni Georgetown, unajulikana kwa usanifu wa majengo ya kikoloni ya Uingereza, ikijumuisha Kanisa Kuu la Kianglikana refu la St.George's Anglican Cathedral.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi nchini Guyana, inadaiwa Ramdeen alinaswa na umeme usiku wa kuamkia Desemba 2, 2022 akiwa na vijana wengine watatu wakiweka mti wa Krismasi wa chuma wenye urefu wa takribani futi 27 mbele ya makazi ya mwananchi wa huko Lusignan.

Loop imeeleza kuwa, inadaiwa mtaalamu huyo aliyekuwa akiweka mti huo alikutana na waya wa juu ambao ulisababisha kupigwa kwa shoti ya umeme.

Ripoti ya Jeshi la Polisi inasema, Ramdeen na wengine wote walikuwa wakiweka mti wa Krismasi wa chuma kwa kutumia crane iliyounganishwa kwenye gari, ingawa bado uchunguzi unaendelea ili kufahamu chanzo zaidi za tukio hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news