Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani,Mwantum Mgonja tarehe 19 Desemba, 2022 ameongozana na Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatilia maendeleo ya Mradi wa Madarasa 132 ya Mama Samia katika Shule za Sekondari Morogoro, Kazole na Mwinyi ambayo yanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023. Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imepokea kiasi cha shilingi 2.640 bilioni kwa ajili ya madarasa 132 ya sekondari.