FIFA yachapisha video inayoonesha bao la Japan dhidi ya Uhispania kwenye Kombe la Dunia 2022

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limechapisha video siku ya Ijumaa inayoonesha bao la ushindi la Japan dhidi ya Uhispania wakati wa mechi ya Kundi E kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022.

Japan iliishinda Uhispania 2-1 siku ya Alhamisi na pasi ya bao la ushindi ilitolewa kutoka kwenye ukingo wa mstari wa kona. Kulikuwa na madai kwamba mpira ulikuwa tayari nje ya uwanja na bao halikupaswa kuruhusiwa.

Shirikisho hilo la Kimataifa limechapisha picha za kamera za mstari wa goli zilizotumiwa na waamuzi katika mechi hiyo ili kumaliza mijadala kuhusu nafasi hiyo.

"Bao la pili la Japan katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Uhispania lilikaguliwa na VAR ili kubaini kama mpira ulikuwa haujatinga," FIFA iliandika kwenye Twitter. "Maafisa wa mechi ya video walitumia picha za kamera za mstari wa goli ili kuangalia kama mpira ulikuwa kwenye mstari au la."

Samurai Blues waliwashinda mabingwa wawili wa zamani wa Dunia, Ujerumani na Uhispania, katika kundi hilo na kutinga Raundi ya 16 wakiwa vinara wa kundi kwa pointi sita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news