NA DIRAMAKINI
WATAHINIWA 540 wanaotoka katika vituo sita vya Joylanda, Castle hill, Green Acress, Maktaba, Great Vision na Mtendeni jijini Dar es Salaam wamezuiwa matokeo ya darasa la saba baada ya kubainika kufanya udanganyifu.
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limeeleza leo Desemba Mosi, 2022 kuwa
matokeo ya watahiniwa hao yanazuiwa hadi uchunguzi juu ya tuhuma hizo utakapokamilika.
“Wakibainika kufanya udanganyifu matokeo yao yatafutwa kwa mujibu wa kifungu Na. 4(8) cha Kanuni za Mitihani 2016 na endapo hawatabainika kufanya udanganyifu watapewa matokeo yao".
Pia NECTA linazuia matokeo ya watahiniwa 179 ambao waliugua au walipata matatizo na kushindwa kufanya mitihani kwa masomo yote au baadhi ya masomo.
“Watahiniwa hudika watapewa fursa nyingine ya kurudia kufanya mtihani wa Kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2023 kwa mujibu wa kifungu 32(1) cha Kanuni za Mitihani;