NA DIRAMAKINI
WANAFUNZI 1, 073, 941 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 wakiwemo wavulana 514, 846 na wasichana 559, 095 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 14, 2022 na Waziri wa Ofisi ya Rais- Tamisemi, Angellah Kairuki.
Amesema kuwa, idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2023 imeongezeka kwa wanafunzi 166, 139 sawa na ongezeko la asilimia 18.30 ikilinganishwa na wanafunzi 907, 802 walopata alama ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.
WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023 bonyeza Mkoa wako
Aidha,kati waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2, 775 sawa na asilimia 0.26 ambao kati yao wavulana ni 1, 491 na wasichana 1, 284.