NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)-NEC imepitisha majina ya wagombea 374 kuwania ujumbe wa ya wagombea wa ujumbe wa NEC.
Wagombea hawa watachuana kuwania viti 30 kwa maana ya 15 Tanzania Bara na 15 Zanzibar katika mkutano mkuu wa CCM unaoanza leo Desemba 7 hadi 8,2022.
Kikao cha kuchuja majina ya wagombea zaidi ya 2,000 kimefanyika Desemba 6, 2022 chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tanzania Bara wamepitishwa wagombea 251 watakaowania nafasi 15. Kati ya hao 251, wanawake ni 79 na wanaume 172.
Miongoni mwa majina ya wagombea zipo sura mpya ambapo mwandishi wa habari, Rose Mweko jina lake limechomoza.
Rose Mweko ni kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amewahi kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama kwa nyakati tofauti na bado akaendelea kuwa mtulivu. Rose Mweko 2015 aligombea ubunge Jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma katika kura za maoni kura hazikutosha
Aidha, mwaka 2017, Rose Mweko aligombea ujumbe Baraza Wazazi Mkoa wa Geita na kuibuka mshindi ambapo alikua Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Geita na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Mkoa wa Geita.Mwaka 2020 aligombea ubunge viti maalum Mkoa wa Geita kura hazikutosha.
Miongoni mwa sifa za kipekee alizonazo Rose Mweko ni kuwa mchapakazi,ucheshi, mnyenyekevu na mshauri mzuri.
Pia,Rose Mweko ana jicho la tatu katika kun'gamua jambo na ni mtulivu katika kuchukua maamuzi.Wajumbe tumchague Rose Mweko, dada mwenye ujasiri, shupavu na hakika anafikika na kutumika bila shida.