Joseph Ntakarutimana kutoka Burundi ndiye Spika mpya EALA

NA DIRAMAKINI

JOSEPH Ntakarutimana ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Burundi cha Conseil National de Défense de la Démocratie-Forces pour la Défense de la Démocratie (CNDD-FDD) amechukua nafasi ya aliyekuwa spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Martin Ngoga kutoka nchini Rwanda.
Ntakarutimana alishinda baada ya wanachama 54 kati ya 63 kumpigia kura, huku kura nane zikiharibika na moja haikupigwa. Ili mtu ashinde nafasi ya Uspika wa EALA, lazima apate angalau kura 42.

Sudan Kusini ilikuwa imesajili wagombea watatu kuwania nafasi hiyo, lakini walijiondoa usiku wa kuamkia uchaguzi huo na kumwacha Ntakirutimana bila kupingwa.

Uchaguzi huo umefanyika Desemba 20, 2022 ikiwa ni safari ya Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) jijini Arusha.

"Tuligundua kuwa Burundi ilijiunga na EALA kabla yetu na tuliamua, kwa umoja na kufanya kazi pamoja, kuiruhusu Burundi kupita. Uamuzi huu utaleta maelewano na 2027, Burundi itatuunga mkono,”alisema Dkt.Ann Itto, mmoja wa wagombea wa Sudan Kusini.
Aidha, uchaguzi huo umesimamiwa na Katibu wa Bunge la EALA, Alex Obatre ambaye alitoa nafasi kwa wagombea hao waliojitoa kutamka kwa vinywa vyao kuwa wameridhia kufanya hivyo bila kushinikizwa.

Spika mpya Ntakirutimana alijiunga na Bunge la Burundi mwaka 1993 na alikuwa amehudumu nafasi hiyo kwa miaka 30 iliyopita.

"Hapa ndipo mahali (Arusha) ambapo tulitia saini makubaliano ya nchi yangu ...yalinifanya kuwa msafi na mkimbizi (kuwa) mbunge," alisema Spika mpya wa EALA Ntakirutimana.
Aidha, kiongozi huyo anakuwa spika wa sita wa Bunge la Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Martin Ngoga wa Rwanda ambaye muda wake ulimalizika Desemba 17,mwaka huu.

Bunge hilo linaundwa na nchi wanachama saba ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudani Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news