Kampuni ya Barron yawasilisha msaada wa viatu kwa watoto wenye maambukizi ya VVU

NA DIRAMAKINI

KATIKA kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani leo Disemba Mosi, 2022 Kampuni ya Barron ambao ni wazalishaji na wauzaji wa viatu vya watoto wa shule, wameshiriki kutoa msaada wa viatu jozi 50.
Viatu hivyo vimetolewa kwa watoto wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi viatu hivyo kwa watoto hao, Mkurugenzi wa Kampuni ya Barron Group, Bi.Jacqueline Kawishe amesema kuwa viatu hivyo vimetolewa na mdau ambaye hakutaka jina lake litajwe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mapambano ya serikali dhidi ya UKIMWI.
Bi.Kawishe amesema kuwa, zawadi hizo zimetolewa kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani zikiambatana na kauli mbiu isemayo, "Mpange Mwana, Twende Sawa, Imarisha usawa Kujilinda ni ibada".
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt.Delila Moshi, msimamizi wa masuala ya UKIWMI katika hospitali ya Mnazimoja, Dkt.Vivian Vesso pamoja na mtawala mkuu wa masuala ya UKIMWI katika hospitali ya Mnazimmoja, Dkt.Zainabu Mwinyimkuu wamempongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Barron Group, Bi.Jacqueline Kawishe na wadau mbalimbali nchini kwa kuendelea kujitolea kwa watoto wenye mahitaji mbalimbali hususani watoto wenye maambukizi ya UKIMWI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news