BIBI TITI MOHAMED, alikuwa ni mwanaharakati na shujaa aliyepigania Uhuru. Alipambana na alifanya kila njia akisaidiana na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Historia yake na harakati za kudai uhuru ni pana na bila shaka inagusa wengi kwa jinsi mwanamke anavyoweza kuwa jasiri na kukubali kuweka rehani kila kitu kwa ajili ya kuipatia uhuru wa Tanganyika.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Rufiji chini ya Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa inakuletea Bibi Titi Memorial Festival kuanzia Desemba 14 hadi 15,2022 katika Uwanja wa Ujamaa Rufiji.