Luis Suarez akilia huku Uruguay ikiaga michuano ya Kombe la Dunia 2022

NA DIRAMAKINI

LUIS Suarez ameshindwa kuzuia machozi wakati Uruguay ilipotolewa katika Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linaloendelea nchini Qatar, kwa mtindo wa ajabu.

Luis Suarez akilia benchi. (Picha na Gettyimages).

Licha ya kuifunga Ghana katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi H, timu hiyo ya Amerika Kusini inarejea nyumbani mapema kwani ushindi wa dakika za lala salama wa Korea Kusini dhidi ya Ureno ulitosha kuwavusha.

Korea Kusini ilionekana kuwa ndiyo itakayoongoza mchezo wa mapema kabla ya Son Heung-min kucheza pasi nzuri kwa Hwang Hee-chan na kufunga bao dakika ya 91.

Habari za bao la Korea Kusini zilipomfikia Suarez kwenye benchi baada ya kubadilishwa alijua nchi yake ilikuwa inatoka kwenye mashindano licha ya juhudi zao dhidi ya Ghana.

Ikiongoza kwa mabao 2-0, Uruguay ilihitaji bao lingine, kutokana na Korea Kusini kuwazidi Ureno mawili. Lakini pamoja na juhudi zao nzuri haikuwa hivyo na Suarez hakufarijika kwa muda wote.

Akiwa na umri wa miaka 35, mshambuliaji huyo anajua hilo litakuwa Kombe lake la mwisho la Dunia na alihuzunishwa sana na jinsi lilivyomalizika.

Suarez ambaye aliisaidia timu yake kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza alionekana akitazama kwa wasiwasi akiwa benchi baada ya kufanyiwa mabadiliko huku wachezaji wenzake wakijaribu kufunga. Ghana ilionesha ushujaa wa hali juu ambao uliwawezesha kuzuia majaribio kadhaa.

Kutoka Kundi H Ureno na Korea Kusini zimesonga mbele.Kwa Uruguay, fowadi Giorgian de Arrascaeta alifunga mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza.

Ureno wamesonga mbele katika kundi hilo wakiwa na alama sita, Korea Kusini alama nne. Huku Uruguay ikiondolewa kwa kuwa na alama nne ingawa tofauti ya mabao na Korea Kusini na Ghana wameaga wakiwa na alama zao tatu katika kundi hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news