Majengo ya maghorofa kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa Tunduma

NA DIRAMAKINI

UHABA wa madarasa katika Halmashauri ya Mji Tunduma mkoani Songwe umetajwa kumalizika baada ya ujio wa madarasa yanayo jengwa kwa mtindo wa ghorofa hali iliyotajwa kuondoa msongamano uliopelekea wanafunzi kushindwa kusoma vizuri.
Kutokana na msongamano huo wa wanafunzi, Halmashauri ya Mji Tunduma kupitia vikao vyao walipendekeza kuanza kujenga shule kwa mfumo wa Maghorofa ili kuendana na uhaba wa maeneo kutokana na Mji huo ambao ni wa kibiashara kuingiwa na watu wengi ambao wamekuwa wakifuata fursa za kibiashara.

Zephania Mgola mkuu wa shule ya sekondari Uwanjani, alisema ili kukabiliana na changhamoto hiyo mwezi Disemba 28, 2021 walipokea sh. 470,000,000 kutoka Serikali Kuu kupitia Program ya SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Uwanjani.
Alisema ujenzi huo ulianza Mwezi Machi 18 mwaka 2022, ukihusisha ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika jengo la Ghorofa, vyumba vitatu vya maabara za sayansi, jengo la utawala Pamoja na jengo la ICT na Maktaba.

“Mpaka sasa mradi umepokea Tshs. 768,709,612 na kutumia Ths. 662,305,847,000 ambapo matumizi ya fedha hizo yamehusishwa manunuzi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi Pamoja na malipo ya mafundi katika hatua mbalimbali za kazi walizozifanya,” alisema Mwalimu Kigola.

Kigola alisema wana kila sababu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suruhu Hassan kwa kukubali kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Songwe, Bi. Happines Seneda alisema ni jambo la busara kupongeza kazi ya Rais Samia kwa kutoa fedha hizo na kwamba kazi iliyopo ni kuhakikisha wanaongeza juhudi za ufundishaji ili wanafunzi waweze kupata alama A na B.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news