NA LWAGA MWAMBANDE
1. Katika amri kuu, ambazo tunazipata,
Ya kwanza Mungu mkuu, kumshika twatakata,
Na ya jirani ni kuu, elimu tunaipata,
Kuwaheshimu wazazi, hilo jambo kubwa sana.
2. Wamefanya jambo kuu, somo kwetu tumepata,
Ni ile heshimu kuu, wazazi wameipata,
Ndo maana wako juu, Baraka wanazipata,

3. Morocco kwetu wakuu, heshima kwao twapata,
Afrika iko juu, nafasi hiyo kupata,
Kweli tumepanda juu, kama kuvunja ukuta,

4. Nusu fainali kuu, jambo jipya tumepata,
Afrika sasa juu, hata bila ya utata,
Wa mbio za kirikuu, tayari walishatota,

5. Wakifanya jambo kuu, kama goli wamepata,
Wanarukaruka juu, na wengine kuwapita,
Lengo kwenda kwa wakuu, wazazi kuwatafuta,

6. Picha zao ziko juu, wazazi wakikumbata,
Na mabusu juujuu, mengi yamepitapita,
Hiyo ni heshima kuu, wazazi wameipata,
Kuwaheshimu wazazi, hili jambo kubwa sana.
7. Na kuangalia juu, heshima Mungu apata,
Yatokeayo makuu, hawajawahi kupata,
Hayo ni mambo makuu, elimu kwao twapata,

8. Wengi hapa na majuu, wanafunga wanapeta,
Heshima ile ya juu, vitu vingine hupata,
Hili kwetu somo kuu, wazazi kutowapita,

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602
IKICHUKUA eneo la takribani kilomita za mraba 11,437, Qatar ni mojawapo ya mataifa madogo ya Kiarabu. Ina mpaka mmoja tu wa ardhi, na Saudi Arabia eneo la Kusini. Aidha, Qatar inashirikiana mipaka ya baharini na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain.
Kiarabu ni lugha rasmi, lakini Kiingereza na Kifaransa ni miongoni mwa lugha zinatomuiwa mara nyingi na wageni wenyeji kutoka nje.
Kiutawala, Qatar inajumuisha manispaa nane ikiwemo Al Shamal, Al Khor, Al Shahaniya, Umm Salal, Al Daayen, Ad Dawhah (Doha), Al Rayyan, na Al Wakrah.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema, baada ya siku 28 za Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kufikia tamati, masomo aliyojifunza kwa Qatar yanamshawishi kuhamasisha siku zijazo wapewe tena fursa ya kuandaa michuano mikubwa ya Dunia. Endelea;