Mbappe awagomea wauzaji pombe, wadhamini Kombe la Dunia nchini Qatar

NA DIRAMAKINI

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain na timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé Lottin (Kylian Mbappe) amekataa kupiga picha mbele ya nembo ya kinywaji chenye kilevi kikali cha Budweiser.

Mbappe akiwa ameziba nembo ya Budweiser wakati wa picha.
 
Ni katika michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 nchini Qatar.

Ripoti zinasema kuwa, nyota huyo wa Ufaransa hataki kuhusishwa na Budweiser, mmoja wa wadhamini wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 na alificha kwa makusudi jina la chapa hiyo kwenye picha za mchezaji bora wa mechi.

Mbappe bado hajaonekana katika mkutano na waandishi wa habari nchini Qatar katika juhudi za kuepusha maswali kuhusu mustakabali wake na Paris Saint-Germain.

Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), ambalo limempa Mbappe uungwaji mkono wakati wa kususia mkutano na waandishi wa habari, wameamua kulipa faini yoyote ya FIFA.

Inaelezwa kuwa, Mbappe ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wengi wa Ufaransa kufuatia ustaa wake katika soka, hataki kuharibu taswira yake kwa kuendeleza unywaji wa pombe kali aina ya Budweiser.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliongeza kuwa, Shirikisho la Ufaransa halipaswi kulipia uamuzi wake wa kibinafsi na atatoa faini yoyote.

Nyota huyo wa Ufaransa amecheza akiwa na mabao matano na pasi mbili za mabao katika michezo minne hadi sasa katika Kombe la Dunia la FIFA la 2022 nchini Qatar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news