Mheshimiwa Sagini ashiriki ibada, harambee ya Kanisa la Waadventisa Wasabato Lugalo

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Jumanne Sagini ameshiriki ibada katika Kanisa la Waandventista Wasabato la Lugalo lililopo Mtaa wa Ukwamani Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Sambamba na kusimamia zoezi la harambee katika kanisa hilo yenye lengo la kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la ibada lililoanza kujengwa kanisa hapo.
Harambee hiyo imefanyika Desemba 3, 2022 ambapo Mheshimiwa Sagini aliongozana na viongozi wa kiserikali ambao ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Maduhu Kazi.
Mbunge wa jimbo la Busanda, Mheshimiwa Tumaini Magesa na mwenyeji wao mwenyekiti wa mtaa wa Ukwawami lilipo kanisa hilo, Hamisi Rashindi Chilembe.
Naibu Waziri Sagini amewapongeza Waadventista Wasabato kwa namna wavyounga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga vituo vyao vya afya na shule kwani hiyo inasaidia pia kutoa huduma kwa jamii.

Pamoja na hayo amesema, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Msajili Mkuu wa taasisi za kidini wanayo kampeni ya uhakiki wa makanisa na misikiti yote waliyokwishasajili ili kutambua kama bado wako hai wakiendelea na majukumu yao na kutaka kubaini changamoto wanazozipitia.
Katika hatua nyingine Mheshimwa Sagini ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mheshimiwa Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuwajali wavuvi kwa kuwapa mikopo isiyo na riba.

Ambapo hatua hiyo amesema ni dhamira njema ya serikali katika kuhakikisha wavuvi wanaendesha shughuli zao kwa ufanisi na mafanikio, na hivyo kuwawezesha kupiga hatua za maendeleo.
Pia, kutoa pesa katika mikoa kumi na nne zitakazosaidia ujenzi wa vyuo vikuu kwani hiyo itaongeza chachu ya elimu ya juu katika nchi yetu na kulifanya taifa liwe na wasomi wengi watakaoleta mageuzi ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news