NA DIRAMAKINI
LEO Desemba 3, 2022 wadau mbalimbali wameshiriki katika Mjadala wa Kitaifa ulioangazia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na Maendeleo ya Mikoa ya Kusini kwa maana ya Lindi na Mtwara. Katika mjadala huo, washiriki wamesema haya;
"Rais Dkt.Samia toka ameingia madarakani ameamua kufufua matumaini ya gesi, kwa mara ya kwanza ametangaza tunaenda kusaini makubaliano ya mradi wa gesi unaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 70, ambapo zaidi ya watu elfu 10 wataajiriwa kwa wakati mmoja, hili la gesi watu wa Kusini limewapa faraja kubwa sana.
"Kwa mwaka huu fedha Rais Dkt.Samia ameleta zaidi zaidi shilingi bilioni 110 kwa ajili ya pembejeo, hili jambo limeiondoa korosho kwenye ICU, nataka kufikiria bila hili la pembejeo hali ya korosho ingekua mbaya sana, kwenye korosho Rais Dkt.Samia amefanya mambo ya msingi sana.
"Mimi nina vituo vya afya vingi vyenye ubora karibia kila kitu kinamalizika kwenye kituo cha Afya, nikawa namtania Rais inaweza kufikia hatua Hospitali za Wilaya zikawa na upungufu wa wagonjwa kwa sababu Vituo vya Afya vinafanya kila kitu."
MHE. HAMIDA MOHAMMED ABDALLAH, MBUNGE WA LINDI MJINI
"Sisi wanawake viongozi ambao tupo majimboni Rais Dkt.Samia anatupa moyo sana wa kuendelea kufuata nyayo zake na kuendelea kupambana, ili majimbo yetu yawe mazuri na wananchi wetu waweze kupata maendeleo kwenye kila sekta.



DKT.JAMES MATARANGIO, MKURUGENZI MKUU WA TPDC
"Mradi huu wa LNG utazalisha ajira 6000 wakati wa ujenzi na ajira 500 baada ya kukamilika, na kingine watanzania watejengewa uwezo kwa sababu watakua wameshiriki wakati wa ujenzi, lakini Serikali imeahidi itajenga Chuo cha Veta pale Lindi ili vijana wajifunze.
"Manufaa mengine ya mradi huu wa gesi ni kuuzwa nje ya nchi, na kiasi kingine kitauzwa nchini kwa matumizi ya kuzalisha umeme, na matumizi ya majumbani ambapo itasaidia sana kwenye utunzaji wa mazingira kwa wanaokata kuni kwa ajili ya mkaa.
"Hii gesi itakayotokana na mradi wa LNG itaweza kuuzwa Kimataifa hasa kwa nchi za Ulaya na Asia, lakini pia uwepo wa huu mradi utasaidia kukua kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sababu shughuli nyingi zinafanyika hapa."
FRANCIS ALFRED, MWENYEKITI WA BODI YA KOROSHO
"Tandahimba kuna kikundi cha kinamama kinaitwa Tanzania Delicious Cashew wanaandaa Kontena la Korosho ambalo litasafiri kwenda Ujerumani, ndani ya wiki mbili zijazo likikamilika tutalisafirisha, kwa hiyo tutaendelea kuangalia masoko ya korosho.

"Tunahamasisha wabanguaji wa Korosho wa viwanda waweke amba wanauza nje ya nchi waweke MADE IN TANZANIA, ili alama ya korosho yetu isiweze kupotea kwa sababu Korosho inayotoka Tanzania ni bora kuliko za nchi nyingine hivyo ikijulikana ni korosho yetu itatupa masoko mengi zaidi."
DKT. BENSON NDIEGE, MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA NA MTENDAJI MKUU TUME YA MAENDELEO NA USHIRIKA
"Kwa mwaka uliopita wakulima wa Soya walizalisha kilo milioni 5 ambazo wamepata fedha zaidi ya TSH. Bilioni 5, na kwenye mbaazi wamezalisha zaidi ya kilo milioni 6 na wamepata pesa TSH. Bilioni 7 kwenye ufuta wamezalisha kilo milioni 79 na wamepata shilingi bilioni 245.

"Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia imeboresha sana mifumo ya ushirika na ndiyo maana siku hizi husikii kelele tena kuwa mkulima amepoteza mazao yake, lakini pia Serikali inaendelea na ujenzi wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia mazao."