Musoma Vijijini waanza kutembea kifua mbele kwa huduma ya maji safi na salama

NA FRESHA KINASA

KAMA ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuimarisha huduma ya upatikaji wa maji kwa ufanisi,wananchi zaidi ya 8,000.wa vijiji vya Chitare na Makojo katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama. Hatua hiyo ni kufuatia Serikali kupitia Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutekeleza mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja,fedha ambazo ni kutoka Mfuko wa Maji wa Taifa.

Wameyasema hayo wakati wakitoa shukurani zao na pongezi kwa Rais Dkt.Samia na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo kwa kuwezesha mradi huo ambao wamesema ni mkombozi kwao ambapo kwa sasa wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.
"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mradi huu muhimu wa maji pia pongezi kwa Mbunge wetu Prof. Muhongo kwa usimamizi na ufuatiliaji madhubuti wa miradi mbalimbali na mradi huu mwanzo hadi sasa kusudi wananchi wake tuondokane na tatizo la maji, hatua hii ni muhimu kwa maendeleo yetu,"amesema Neema Juma.

"Maji ni uhai sote tunajua hivyo. Kwa hiyo kitendo cha Serikali kutusogezea maji karibu na makazi yetu ni kutuwezesha kuweze kufanya kazi za maendeleo kwa ufanisi kwa ufanisi, badala ya kutembea umbali mrefu kwa kutafuta maji muda huo utatumika kwa kufanya uzalishaji mali na shughuli za maendeleo na hii inatusaidia sana wanawake ambao muda mwingi changamoto hii imekuwa ikitukumba pongezi wa mbunge Prof. Mubongo na Rais wetu,"amesema Elizabeth Maira.
Aidha, taarifa ya Jimbo la Musoma Vijijini iliyotolewa leo Desemba 2, 2022 imeeleza kuwa. "Vijiji vya Chitare na Makojo vya Kata ya Makojo vimesubiri maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria tokea mwaka 2013. Ambapo mradi huo ulioanzwa kutekelezwa na halmashauri yetu (Musoma DC) tokea mwaka wa Fedha 2013/2014, sasa unarudiwa na unakamilishwa kwa ubora mzuri na RUWASA," imeeleza na kufafanua,

"RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa Wanakijini wa Chitare wameanza kupata maji safi na salama ya bomba. Kwa muda mfupi ujao, Wanakijiji wa Makojo nao watapata maji ya bomba hilo."imesema.

"Tumeomba bomba hilo lijengwe hadi Kijiji cha Chimati ambacho nacho kiko ndani ya Kata ya Makojo. Serikali imepokea ombi letu na kukubali kulitekeleza. RUWASA inaendelea kufanya kazi zenye ubora mzuri ndani ya jimbo letu."imebainisha taarifa hiyo.
Kwa upande waka Mhandisi Innocent Edward kutoka Ofisi ya Meneja wa (RUWASA) Wilaya ya Musoma amesema, mradi huo unagharama zaidi ya shilingi bilioni moja na fedha zimetoka Mfuko wa Maji wa Taifa na kwamba wakazi wapatao 8,500 wa vijiji hivyo utawanufaisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news