NA DIRAMAKINI
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Bw.Fadhili Ngajilo amewatakia maandalizi mema na sherehe njema za Sikuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wananchi wote wa Mkoa wa Iringa na Watanzania kwa ujumla.
Ngajilo amewataka Watanzania kusherehekea sikukuu hizo kwa utulivu na amani na kuwataka kujiwekea malengo thabiti ambayo yatawawezesha mwaka 2023 kuyafikia malengo na ndoto zao.
"Pia nichukue nafasi hii kuwaomba wazazi na walezi kuhakikisha kuwa, wanafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuwawezesha watoto wao kwenda shule kwa wakati. Litakuwa jambo la heri kila mmoja akiweka malengo kwa mtoto wake kwenda shule.
"Tunaona namna ambavyo Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita, hii ni hatua njema...lazima tuunge mkono juhudi hizi.
"Hivyo tufunge mwaka kwa heri na tufungue mwaka kwa heri kwa kuhakikisha tunaendelea kutekeleza majukumu yetu ambayo yatawezesha kufanikisha malengo yetu na kuliwezesha Taifa kusonga mbele kiuchumi, kikubwa Kazi iendelee iwe mijini au vijijini. Kwa mara nyingine niwatakieni tena heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2023,"amesema.