Rais Dkt.Mwinyi:Hayati Jiang Zemin atakumbukwa daima

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefika Ofisi za Ubalozi mdogo wa China uliopo Mazizini jijini Zanzibar na kutia saini kitabu cha maombolezo kutokana kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa China, Jiang Zemin (96).
Katika salamu zake Dkt.Mwinyi amesema, amepokea kwa masikitiko na huzuni taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa China Hayati Jiang Zemin, aliyefariki dunia Novemba 30, 2022 kutokana na sababu za ugonjwa wa saratani ya damu.
Amesema, kwa niaba yake na wananchi wa Zanzibar, anatoa mkono wa pole kwa Rais wa China Xi Jinping na wananchi wote Taifa hilo kwa kuondokewa na kiongozi wao na kumtaja hayati Zemin kuwa alikuwa nguzo muhimu ya uongozi wa Taifa hilo, aliyeweka misingi imara ya kiuchumi, umoja pamoja na mshikamano.

Amesema Komredi Jiang Zemin atakumbukwa kwa kuwa kiongozi bora na Mwanamapinduzi, aliyekuwa chachu ya ushirikiano kati ya China na Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyika kazi zake Zanzibar, Mhe. Zhang Zhisheng baada ya kumaliza kutia saini kitabu cha maombelezo kufuatilia kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa China Jiang Zemin, leo Desemba 2, 2022 katika ubalozi mdogo wa China Mazizini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Pia amesema, Hayati Zemin atabakia daima katika kumbukumbu kwa kuzingatia ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Taifa hilo na Zanzibar na Tanznaia kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news