NA DIRAMAKINI
KATIKA kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali.
Mosi, amesema wafungwa wenye sifa stahiki wapunguziwe robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 58.
"Wafungwa hao sharti wawe wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili au zaidi ambao wametumikia robo ya adhabu zao gerezani na wawe wameingia gerezani kabla ya Septemba 10, 2022 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2 (i-x);

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Desemba 10, 2022 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.
"Pili wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo kwenye hatua ya mwisho "terminal stage". Ugonjwa na hatua hiyo vithibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya.
"Na tatu ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao wametumikia robo ya adhabu zao, Umri huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya;