Rais Dkt.Samia, Dkt.Mwinyi,Kinana wavunja rekodi ushindi CCM, Mawaziri wang'ara NEC

NA DIRAMAKINI

RAIS mstaafu wa Zanzibar, Dkt.Ali Mohamed Shein ambaye ni msimamizi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemtangaza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine.

Dkt.Samia amepata ushindi huo baada ya kupigiwa kura za ndio 1914 kati 1915 kupitia uchaguzi uliofanyika leo Desemba, 7, 2022 jijini Dodoma.

Pia Dkt.Shein amemtangaza Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara baada ya kutetea nafasi hiyo.

Kanali mstaafu Kinana ametetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za ndio 1913 kati ya 1915 kupitia uchaguzi huo jijini Dodoma.

Wakati huo huo, Dkt.Shein amemtangaza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, baada ya kupigiwa kura za ndio 1912 kupitia uchaguzi huo ambao viongozi hao walikuwa wakigombea nafasi hizo peke yao.

Katika hatua nyingine,idadi kubwa ya nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa zimechukuliwa na mawaziri akiwemo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Angelah Kairuki.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezekezaji, Dkt.Ashantu Kijaji, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula wakiwa ni kwa uchache.
 
Katika hatua nyingine, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wamewatosa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), George Simbachawene pamoja na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ofisi Rais (Utumishi na Utawala Bora), Deo Ndejembi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Jumanne Sagini.

Wengine ni Waziri wa zamani wa Kilimo, Japhet Hassunga na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba,Mudhihir Mudhihir na mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.
 
 
WANAWAKE


1. Dkt.Angelina S Mabula Kura 770


2. Dkt.Ashatu Kijaji Kura 764


3. Christina Solomon Mndeme Kura 761


4. Hellen Makungu Kura 755


5. Fenela A. Mukangara Kura 747


6. Angellah J. Kairuki Kura``` 730


WANAUME
1. Mahenda Leonard 845


2. Bashungwa Innocent 720


3. Wasira Steven 680


4. Msome Jackson William 591


5. Kasheku Msukuma 587


6. Kasesela Richard 574


7. Wambura Chacha Mwita 545


8. Bashe Hussein 510


9. Nnauye Nape Mosses 508


10. Gwajima Josephat 497


11. January Makamba 452


12. Mwigulu Nchemba 450


13. Macha 435


14. Msengi Ibrahimu 428

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news