Safari 7,000 za ndege zarekodiwa wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Qatar

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga ya Qatar (QCAA) imetangaza kuwa, wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Qatar 2022 ilirekodi zaidi ya safari 7,000 za ndege.

QCAA imebainisha kuwa,viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Hamad na Doha vilishuhudia ongezeko kubwa tangu kuanza kwa mashindano hayo.

Katika taarifa iliyotolewa na QCAA imesema kuwa, wasafirishaji wengi wa Ghuba walianza safari za ndege hadi Qatar. Aidha, mashirika ya ndege kutoka nchi za Kiarabu na kwingineko duniani yameongeza huduma zao hadi Doha ili kutoa usafiri wa anga uliounganishwa kwa mashabiki wa mashindano.

QACC imethibitisha kuwa, mashirika kadhaa ya ndege ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Lufthansa ya Ujerumani, Air France, Finnair, na KLM, pamoja na mashirika ya ndege kutoka Amerika Kusini na Afrika, yameanza kufanya safari za kawaida na za kukodi kwenda Qatar, hali ambayo imesababisha ongezeko kubwa la usafirishaji kati ya Qatar na kwingineko duniani.

Picha na arabianbusiness.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news