Serikali Kuu yafanya jambo wilayani Same

NA OR-TAMISEMI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imekamilisha ujenzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Dharura lililojengwa katika hospitali ya wilaya hiyoJengo hilo lililogharimu shilingi milioni 300 limejengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu na ni miongoni mwa majengo ya wagonjwa wa dharura 80 yaliyojengwa katika vituo vya kutolea huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumzia ukamilishaji wa jengo hilo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, Dkt. Alex Philemon amesema, kuanzia mwaka 2023 wananchi wa Same na maeneo ya jirani wataanza kufaidika na huduma za dharura.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Same, Dkt.Ibrahimu Sembua amesema, hapo awali walikuwa wanatoa huduma za dharura kwenye jengo la wagonjwa wa nje ambapo huduma hiyo haikuwa inatolewa kwa mpangilio mzuri, lakini kwa upatikanaji wa jengo hilo huduma zitakuwa za uhakika. 

Naye Afisa Muuguzi wa Hospitali ya wilaya hiyo, Azania Thabiti amesema, Wilaya ya Same ipo kwenye barabara kuu ambapo ajali hutokea mara kwa mara na walikuwa wanaletwa katika hospitali hiyo kwa kuwa hapakuwa na jengo hilo iliwalazimu kuwapeleka Mawenzi au KCMC, lakini kwa sasa watawahudumia katika jengo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news