Serikali yaanza rasmi kuhudumia wagonjwa wa dharura Nzega Mji

NA OR-TAMISEMI

HUDUMA za wagonjwa wa dharura zimeanza kutolewa rasmi katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora baada ya jengo la EMD kukamilika.

Jengo hilo ni miongoni mwa majengo 80 yanayojengwa kwenye Hospitali za Wilaya nchini kote ambapo limekamilika kwa asilimia 95 na kuanza rasmi kutoa huduma.
Akizungumzia ukamilishaji wa jengo hilo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Dkt. Jabir Juma Msuni amesema shilingi milioni 300 zimetumika kukamilisha jengo hilo muhimu ambalo litadaidia kuongeza ubora wa huduma za dharura katika wilaya pia.

"Uwepo wa huduma za dharura utarahisisha utendaji kazi wa watumishi na kuongeza imani kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali yetu,"amesema Dkt.Jabir.

Pia ameeleza kuwa, uwepo wa huduma hizo za dharura zitasaidia kuokoa maisha ya watu kirahisi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania yamejengwa Majengo ya Huduma za Dharura (EMD) 80 pamoja na Majengo ya Huduma za Wagonjwa Mahututi (ICU) 25 kwenye Halmashauri za kimkakati.

Jumla ya shilingi Bilioni 226 zimetumika katika ujenzi wa majengo hayo kwenye utoaji wa huduma za afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news