Serikali yasisitiza faida za lishe bora nchini

NA FRESHA KINASA

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amesema kwamba taifa linahitaji watu wenye afya watakaofanya kazi za uzalishaji na maendeleo hivyo suala la lishe bora lazima lipewe mkazo na kusimamiwa kikamilifu kuanzia ngazi ya familia huku wanaume akiwahimiza kulipa kipaumbele jambo hilo katika bajeti za familia zao.
Ameyasema hayo leo Desemba 5, 2022 wakati akizindua Mkutano Mkuu wa Nane wa mwaka wa wadau wa lishe nchini unaofanyika Mjini Musoma mkoani Mara kwa siku mbili kuanzia leo hadi Desemba 6, 2022.

Katika mkutano huo,wadau wa lishe kutoka mikoa mbalimbali wamehudhuria ili kujadili masuala mbalimbali ya lishe chini ya kauli mbiu isemayo 'Kuongeza kasi katika kubooresha hali ya lishe kwa maendeleo ya rasilimali watu na uchumi'.
Amesema kuwa, katika kupambana na tatizo la lishe Serikali imekuwa ikifanya mikakati mbalimbali ambayo inawezesha kukabiliana nalo ikiwemo hatua ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kusaini mikataba ya lishe na Wakuu wa Mikoa yote nchini katika kuhakikisha kwamba makundi yote muhimu yanapata lishe bora.

Amesema, iwapo wanaume watakuwa na msukumo na ushiriki chanya katika jambo la lishe bora itasaidia kwa kiwango kikubwa kuleta ufanisi kwani wao ndio wapangaji wakuu wa bajeti za familia na kwamba badala ya kuweka bajeti katika maendeleo pekee Kama vile ujenzi wa nyumba. Pia wawe na bajeti ya lishe katika familia zao.
Amesema, suala la lishe lazima liimarishwe kwa makundi ya watoto wadogo, wajawazito, na watu walio katika umri wa kuzaa pamoja na makundi maalum katika kuhakikisha kwamba wanakuwa na lishe bora kwa kuzingatia lishe bora.

Ameongeza kuwa, kwa takwimu za mwaka 2018, hali ya lishe imeendelea kuimarika kwa kupungua tatizo la utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 34.7 mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 mwaka 2018 na hivyo kupanda kwa asilimia 3.
Pia, amesema takribani watoto milioni 3 nchini wameathirika na tatizo la udumavu ambapo amesema tatizo hilo linaathari kukua kwenye akili inakuwa changamoto. Hivyo juhudi za pamoja lazima zifanywe kulikabili.

Ameitaja mikoa 11 nchini ambayo inaidadi ya udumavu kuwa ni pamoja na mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Mara, Kagera, Geita, Kigoma, Pwani, Mbeya, Morogoro, Tabora na Dodoma.
Katika hatua nyingine, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imetoa miche 300 ya matunda ili ipandwe katika shule mbalimbali za Manispaa ya Musoma ikiwa ni hatua ya kuunga mkono kuwezesha kupata lishe mchanganyiko na kuondokana na utapiamlo.

Ambapo Naibu Katibu Mkuu huyo na viongozi mbalimbali kutoka Wizara hiyo na serikalini wameshiriki kupanda miche ya matunda katika Shule ya Msingi Mwisenge iliyopo Mjini Musoma aliyosoma Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kuenzi mchango wake katika suala la utunzaji wa mazingira.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt.Halfan Haule ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kwa kutoa hamasa ya upandaji wa miche ya matunda na mbogamboga.

Ambapo ameiagiza Manispaa ya Musoma zoezi la kupanda miche hiyo ya matunda likamilike kabla ya Desemba 8,2022, ambapo shule sita za Manispaa hiyo ikiwemo Mwisenge,Mtakuja, Nyarigamba A. Nyarigamba B, Nyabisare na Nyarusurya na kila shule imepata miche 50.
Dkt. Germana Leyna ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya chakula na Little amesema wanatambua vijana wanaweza kuwa chachu katika kusaidia Serikali kupambana na lishe duni hivyo kupitia Miche hiyo kupandwa katika shule itawapa mwamkoa na kuwa mabalozi kwa jamii.

Ameongeza kuwa, asilimia 58 ya wanawake nchini walio katika umri wa kujifungua wana changamoto ya upungufu wa damu. Hivyo kupitia juhudi za kupanda miche ya matunda na mbogamboga itasaidia kina mama kuachana na dawa wanazopewa hospitalini.
Meya wa Manispaa ya Musoma, Kapteni mstaafu Patrick William Gumbo mbali na kushukuru, amesema watahakikisha miche hiyo wanaisimamia vyema kusudi iweze kukua na kutoa manufaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news