NA DIRAMAKINI
KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imelazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera. Ni kupitia mtanage wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa leo Desemba 21, 2022 katika Dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Matokeo hayo ni ya kusononesha kwa Wekundu hao huku kwa upande wa watani zao Yanga SC wakiendelea kuchekelea, ikimbukwe kuwa, jana Fiston Kalala Mayele amefunga mabao mawili kuiwezesha Yanga SC kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mayele alifunga mabao yake dakika ya 29 na 47 hivyo kufikisha mabao 13 jumla kwenye ligi msimu huu na kuendelea kuongoza kwa mabao matatu ya Moses Phiri wa Simba.
Aliyezamisha jahazi alikuwa ni Fiesal Salum Abdallah (Fei Toto) dakika ya 66 na sasa mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 44 katika mchezo wa 17.

Kwa upande wa mtanage wa leo, timu ya Kagera Sugar ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wake Deus Bukenya dakika 15 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo akiunganisha mpira wa kona.
Aidha, katika dakika ya 39 ya mchezo huo Simba walisawazisha goli hilo likifungwa na mlinzi wa kati wa timu hiyo akipiga kichwa Kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Clatus Chama.
Kipindi cha pili timu zote zilionekana kushambuliana huku Kagera Sugar wakiimarisha safu yao ya ulinzi kwa kucheza kwa umakini mkubwa huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.