Wanafunzi wa Tanzania, China kubadilishana uzoefu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Taasisi ya Ufundi ya Chonqing (CQVIE) kutoka nchini China.
Waziri Mkenda amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka Tanzania ikiwa katika mchakato wa MAGEUZI makubwa katika elimu.

Miongoni mwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo ni kubadilishana Wanafunzi na Walimu (exchange program ) ili kubadilishana uzoefu katika ujuzi wanaopata katika mafunzo.
Pia wanafunzi wanufaika wa programu hiyo watakuwa na sifa za kufanya kazi katika makampuni mbalimbali nchini China.
Prof. Mkenda amesema,Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha ushirikiano huo unadumu na unakuwa endelevu kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news