Wanawake Lindi wajigaragaza chini kwa mahaba ya Rais Dkt.Samia

NA DIRAMAKINI

WANAWAKE mbalimbali kutoka Kata ya Mnazimoja mkoani Lindi wameonesha mahaba yao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujigaragaza chini ikiwa ni ishara ya upendo na kufurahishwa kwao kutembelewa kwenye kata yao.
Tukio hilo la aina yake limetokea kipindi Rais Dkt.Samia ametoka kwenye Tamasha la Siku ya Ukimwi Duniani lililofanyika leo Desemba Mosi, 2022 katika Uwanja wa Ilulu Mkoa wa Lindi akielekea Mkoa wa Mtwara kwa shughuli za kitaifa.
Pia wananchi wamemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwatembelea na kuwasikiliza changamoto zao ambapo pia Mheshimiwa Rais ameahidi atarudi tena mara nyingi kwa ziara rasmi ya kimkoa.
Awali wafuasi wa vyama vikuu vya upinzani nchini kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ACT WAZALENDO Mnazi mmoja mkoani Lindi wameungana na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi katika mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa nyakati tofauti, wafuasi hao wameieleza DIRAMAKINI kuwa, dhamira ya kushirikiana na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watanzania wengine kwa umjumla inatokana na wao kuvutiwa na uongozi shirikishi, sikivu na jumuishi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia.

Pia wameongeza kuwa, Rais Dkt.Samia katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kuimarisha demokrasia, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea na iliyokamilika vijijini na mijini ambayo imekuwa na matokeo chanya kwa ustawi bora wa uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news