NA DIRAMAKINI
WATAHINIWA zaidi ya milioni 1.07 kati ya milioni 1.34 wenye matokeo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.
Kati ya hao wasichana ni 558,825 ambao ni sawa na asilimia 78.91 na wavulana ni 514,577 sawa na asilimia 80.41.
Hayo yamesemwa mbele ya waandishi wa habari na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Athumani Amasi wakati akitangaza matokeo hayo leo Desemba Mosi, 2022 jijini Dar es Salaam.
Amasi alikuwa akizungumzia kuhusu matokeo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6,mwaka huu.
Pia amesema katika matokeo ya mwaka 2021 watahiniwa walikuwa 907,802 sawa na asilimia 81.97 ambapo kitakwimu kuna kupungua kwa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka 2021;