NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Indonesia na Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo Jatmiko.
Mheshimiwa Dkt.Kijaji amefanya mazungomzo hayo na Balozi Jatmiko leo Desemba 6, 2022 katika Ofisi za wizara jijini Dodoma.
Waziri Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania iko tayari kuendeleza ushirikiani baina ya nchi hizo na iko tayari kuwezesha miradi ya uwekezaji hususani katika sekta ya kilimo hasa katika uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao ambayo nchi hiyo imepanga kuyaendeleza kama vile karafuu ili kuongeza ajira na kipato kwa wanzania.
Tags
Habari
Kituo cha Uwekezaji Tanzania
Uchumi na Biashara
Uwekezaji Tanzania
Wizara ya Uwekezaji na Biashara