Waziri Mkuu leo Disemba 08, 2022 ameondoka nchini kwenda Luanda, Angola kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 10 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS). Pichani Mheshimiwa Majaliwa akiagana na viongozi kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).