NA MWANDISHI WETU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea mmomonyoko mkubwa wa maadili ambao umeshika hatamu.
Amesema hayo jana Desemba 17, 2022 alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 75 tangu ulipojengwa msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makarere kilichopo Kampala nchini Uganda. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwanamfalme Abdullah wa Zanzibar mwaka 1948
“Katika hili ningeomba turejee maneno ya maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur‘an tukufu Sura ya 33 Ayah 21 (Quran 33:21) kwamba “Hakika ninyi mnacho kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu”.
Ameongeza kuwa taasisi za elimu, jumuiya za dini, viongozi wa dini na viongozi wa umma wanao wajibu wa kuilea jamii kwa kutoa elimu sahihi ya mazingira sambamba na mafundisho sahihi na endelevu ya dini ili kuiwezesha kutambua na kufuata yote yaliyo mema kama tulivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa yote mabaya yanayomchukiza Mwenyezi Mungu.