YALIYOSISIMUA 2022: Zanzibar, wadau kushirikiana kukabiliana na majanga ya kimaumbile

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na taasisi za Kimataifa katika kukabiliana na majanga ya kimaumbile sambamba na kujikinga dhidi ya maafa yanapotokea nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe.Hamza Hassan Juma ameyasema hayo hivi karibuni huko ukumbi wa Kamisheni ya Maafa, Maruhubi mjini Unguja, kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya mawasilinao na habari kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Alisema, vifaa walivyokabidhiwa vitasaidia kuimarisha ofisi za maafa pamoja na utendaji kazi wataasisi zinazoshirikana na kamisheni hiyo, katika utendaji kazi wao.

Alisema, serikali imetathmini hali ya maafa iliyopita pamoja na kuwataka wadau hao wamaendeleo ahadi ya kuomba fedha za kuwaongezea uwezo taasisi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zikiwemo vikosi vya SMZ, KMKM na vikosi vya Zima moto ambao hushirikiana begakwa bega na kamisheni ya maafa wakati wa majanga yanapotokea.

Alisema, Serikali itaendelea kulishukuru Shirika la Afya Duniani kwa jitihada zake za kuiunga mkono Serikali na kuongeza kuwa WHO sio msaada wao wa kwanza kuisaidia serikali,wanashirikiana na mambo mengi ya maendeleo.

“Serikali itaendelea kushirikiana nanyi na taasisi nyingine za kimataifa kwa lengo la kukabiliana na maafa,”alisema Waziri Hamza.

Aidha, Mhe. Hamza aliiomba WHO kuangalia uwezekano wa kuusaidia Mfuko wa Maafa wa Kamisheni hiyo ambao uko kwenye hatua ya mwisho kukamilika kwake.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkaazi wa WHO Tanzania, Dkt.Zabulon Yotialisema alisema, taasisi ya maafa ni muhimu kuwa na vifaa vya habari na mawasiliano ili kuwapa taarifa wananchi na kuripoti habari za majanga yanapotokea.

Alisema, kitengo cha maafa kinahitaji mawasiliano ili kutunza habari na kuwapa habari wananchi wakati majanga yanapotokea.

“Nafurahi kukabidhi vifaa hivi kwa lengo la kuripoti matukio ya maafa yanapotokea, Zanzibar,”alisema Mwakilishi huyo.

Aidha, aliitaka Kamisheni ya kukabiliana na maafa kuchukua tahadhari mapema kabla majanga hayajatokea ili kujinusuru na athari zitokanazo na majanga hayo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Makame Khatibu Makame aliishukuru WHO kwa hatua yao utekelezaji wa ahadi yao kwenye ugawaji wa vifaa hivyo walioitoa tokea mwaka 2020, ambavyo alieleza vitaunganisha taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na kamisheni hiyo wakati wa maafa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news