NA DIRAMAKINI
FEBRUARI 24, 2022, Urusi iliivamia Ukraine ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mzozo kati ya Urusi na Ukraine ulioanza Febrauri 2014, ukihusisha vikosi vya wanaotaka kujitenga vinavyosaidiwa na Urusi kwa upande mmoja, na Ukraine kwa upande wa pili.
Mzozo huo unahusu hasa hadhi ya Crimea na Donbas ambapo uvamizi huo umesababisha makumi kwa maelfu ya vifo kwa pande zote mbili. Pia vita hiyo, imesababisha mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Sambamba na matokeo hasi ya kiuchumi Duniani yaliyotokana na bei za mafuta na vyakula kupaa kwa kasi zaidi.
Inakadiriwa kuwa Waukraine milioni nane walihamishwa ndani ya nchi yao mwishoni mwa Mei na milioni 7.8 walikimbia nchi hadi Novemba 8, 2022 kutokana na vita hiyo.
Mgogoro huo ulipamba moto zaidi mwezi Februari, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kushindwa na Urusi ikapeleka wanajeshi katika maeneo ya wanaotaka kujitenga Februari 22, 2022 ikiwa ni siku moja baada ya kuitambua Jamhuri ya Watu wa Donetsk na Jamhuri ya Watu wa Luhansk, hapa chini ni sehemu ya picha chache zinazosisimua katika vita hivyo;
Mwanaume mmoja akiwa amejikusanyia bidhaa Aprili 25, 2022 kutoka katika duka lililoungua kufuatia shambulio la Urusi huko Kharkiv nchini Ukraine. (Picha na Felipe Dana/AP).
Watu wakiwa wamejificha chini ya handaki kufuatia milipuko wa bomu Machi 26, 2022 huko Lviv, Ukraine ikiwa ni mwendelezo wa vita kati ya Urusi na Ukraine. (Picha na Nariman El-Mofty/AP).
Baba akiagana na binti yake wa miaka tisa wakati treni iliyokuwa imebeba familia yake Aprili 4, 2022 ikiondoka kuelekea Poland kutoka huko OdesaPetros kwa ajili ya kwenda kupata hifadhi kufuatia vita kati ya Urusi na Ukraine. (Picha na Giannakouris/AP).