NA MWANDISHI WETU
ZAMANI za kale alikuwepo mungu dagoni ambaye alikuwa na umbo la samaki na aliabudiwa na wapagani. Sanamu la mungu dagoni lilivalishwa kofia ya kichwa cha samaki aliyeachama juu ikiwa ni ishara ya kumeza kila fundisho linalotoka juu mbinguni kwa lengo la kuficha ukweli.
Leo kofia ya kichwa cha samaki aliyovaa mungu dagoni inapatikana kwenye maeneo mengi ikiwa ni pamoja na ndani ya nyumba za ibada.
Lakini, walikuwepo pia miungu waliovaa kofia za kichwa cha mbuzi au simba,jicho lilitumika kama alama ya mungu mkuu wa anga. Jicho linaloonekana kwenye noti ya dola moja ya Marekani huwakilisha mungu horus,alikuwepo pia mungu mke aliyepewa jina la ISIS.
Ingawa leo jina ISIS linatafsiriwa kama Islamic State of Iraq and Syria, lakini ukweli ni kwamba jina hilo linatokana na mungu mke wa kipagani aliyeabudiwa miaka mingi iliyopita.
Hata hivyo, mungu ISIS bado anaabudiwa leo ndani ya nyumba za ibada ambapo wengi hawajui kama wanamwabudu. ISIS alivaa kofia yenye pembe mbili za ng'ombe na katikati ya pembe kulikuwa na mduara unaowakilisha jua.
Ingawa ni utambulisho wa mungu ISIS, lakini leo kofia hii inatumika kama nembo zinazowakilisha taasisi mbalimbali, wakati taasisi ya Humanism hutumia nembo hii kama utambulisho wake, shirika la runinga ya Hope Channel hutumia pia nembo hii kama utambulisho wake.
Hapa tunapata ibada kwa miungu wawili ambao ni mungu jua (Ra) na mungu mke ISIS,baadhi wanaweza kuhoji inakuwaje nembo tu iwe na madhara kwa mtumiaji ambaye hana lengo linalowakilishwa na nembo au alama: " By symbols...is a man guided and commanded. The illuminati made use of...a pyramid,or triangle,which has been long known to initiate as a sign of mystics or solar faith.
At the top of that pyramid ,or sometimes at its base,was,and in fact,still is, the image of a separate human eye, which has been various refereed to as the open eye of Lucifer...or the eternal watcher of the world and the human scene, "( rejea ; Peirs Compton,The broken cross P. 10-11) anamaanisha"mtu huongozwa na kuamrishwa kwa kutumia alama, illuminati walitumia piramidi au pembe tatu iliyokuwa ikitumika kwa muda mrefu kama ishara ya imani kwa jua, juu ya piramidi au wakati mwingine chini kumekuwepo na jicho linamuwakilisha Lucifa, au mlinzi wa ulimwengu wa milele na mambo yote ya wanadamu.
Kanisa la kale la Babeli lilikuwa limejichukulia ibada za mungu samaki,kwa mapapa wa madhehebu mbalimbali katika matukio kadhaa wameonekana moja kwa moja kama wawakilishi wa mungu dagoni. Hivyo ilikuwa ni muhimu na lazima kisheria kwa dini zinazoabudu sanamu hasa kwa mapapa, wao lazima wavae alama ya mungu wanayemwabudu.
"Na itakuwa katika siku ile ya dhabihu ya bwana, nitawaadhibu wakuu na wana wa Mfalme ,na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni." [Sefania 1---8].
Berosus anasema; kwenye picha ya dagoni kichwa cha binadamu kinaonekana ndani ya kichwa cha samaki, wakati naye Layard anasema ,kwa suala la maaskofu,kichwa cha samaki kinaunda kofia ndefu juu ya binadamu wakati magamba yake, na mkia unaonekana kama unaanguka chini ukiwa kama vazi, kwa nyuma ukiacha mikono ya binadamu na miguu inaonekana. ( Babylon and Nineveh ,page 343).
Katika hadithi za kale za wababeloni palikuwa na Oannes (mungu wa mawimbi) alikuwa na umbile la chura akiwa na kiwiliwili na kichwa cha binadamu, lakini juu akiwa na kichwa cha samaki kilichoachama mdomo wake, mgongoni ni samaki mwenye magamba na mkia. Wasumeriani walimwita " EA" na kama Oannes ,alikuwa ni nusu samaki na nusu binadamu, aliitwa samaki mkubwa wa mbinguni.
Wafilisti walimwita dagoni, mungu samaki ambaye ametajwa kwenye Biblia (Oannes,part II Vladimir Pakhomov taken from a history of Mesopotamia written in the 3rd century BC by Berosus ,A Babylonian priest).
Kofia ya samaki dagon ilivaliwa na makuhani wa Babeli, mapadri wa Dagon,walivaa kofia sawa ambayo ilivaliwa na Cybele ilionekana kama mdomo ulioachama wa samaki juu ya vichwa vya maaskofu,alikuwa ni nusu samaki nusu binadamu.
Dagoni ametajwa katika biblia takribani kwenye sehemu nane zikiwemo vitabu vya: Yoshua 19:27" kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth- Dagoni nao ukafikilia hata Zabuloni tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto.
Waamuzi 16:23 "kisha wakuu wa wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka dagoni mungu wao, na kufurahi kwa maana walisema,mungu wetu amemtia samsoni adui yetu mikononi mwetu."
1 Samueli 5:2,3,4,5,7, "wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu wakalitia katika nyumba ya dagoni,wakaliweka karibu na dagoni. Na watu wa Ashdodi walipoamka alfajiri siku ya pili kumbe dagoni imeanguka chini kifudifudi,mbele ya sanduku la bwana wakaitwaa dagoni,wakaisimamisha mahali pake tena,hata walipoamka kesho yake asubuhi kumbe dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la bwana na kichwa chake dagoni na vitanga vya mikono yake vyote viwili vimekatwa vipo vimelala kizingitini: dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu."
"Kwa hiyo makuhani wa dagoni na mtu awaye yote aingie vyumbani mwa dagoni,hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya dagoni huko Ashdodi hata leo. Kisha hao watu wa Ashdodi walipoona ilivyokuwa,walisema hilo sanduku la Mungu wa Israel halitakaa kwetu kwa maana mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya dagoni,Mungu wetu."
1Mambo ya Nyakati 10:10" wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao wakakikaza kichwa chake nyumbani mwa dagoni".
Kofia yenye pembe mbili juu inayovaliwa na mapapa wa madhehebu mbalimbali anapokaa kwenye madhabahu na kupokea heshima kutoka kwa Makadinali ni kofia halisi iliyokuwa ikivaliwa na makuhani na mapadri wa dagoni,samaki mungu wa wafilisti na wababeli ( the two Babylon; Alexander Hislop; page 215).
Kwa nini mapapa wa madhehebu tofauti wanavaa kofia yenye mdomo wa samaki aliyeachama mdomo? Ukweli ni kwamba kutokana na historia ya kale,mungu samaki wa wababeli aliyeitwa dagoni ndiye aliyekuwa anaitwa Nimrod, wasomi wengi wamekubali kuwa jina la ibada ya dagoni ilikopiwa kutoka Babeli, ( The two Babylon,Hislop page 215).
"Kwenye ibada zao na katika kumuabudu dagoni makuhani wa dini ya kipagani walivaa vazi ambalo liliundwa kutokana na samaki mkubwa".
Mfumo maarufu wa kuabudu huko Babeli ulikuwa ni kwa mungu dagoni, baadae aliitwa Ichthys au samaki ,zama za wakaldayo mkuu wa Kanisa alimwakilisha mungu dagoni,alikuwa anahesabika asiyeweza kufanya makosa, na alitangazwa kuwa ni mtukufu.
Mataifa yaliyotawaliwa na Babeli yalipaswa kuibusu pete na viatu vya mfalme-mungu wa babeli,nguvu ileile na vyeo sawa vinadaiwa siku hizi kutumika na Dalai Lama wa dini ya Buddhism na Papa.
Mavazi ya wapagani ikiwemo kofia ya samaki na vazi kama joho, vya miaka hiyo kale vilivyovaliwa na mapadri wa dagoni siku hizi vinavaliwa na maaskofu,makadinali na mapapa wa sasa (The wine of Babylon ; page 9).
Kulingana na hadithi za Wamisri,wakati mahakimu walipomkuta Osiris (Nimrod) na kosa la kuiharibu dini ya Adam walimkata mwili wake na kutupa vipande vyake mto Nile ilisemwa kwamba,samaki akala moja ya vipande hivyo na akabadilika umbile lake.
Baadae Isis yaani ( Semiramis) alikuwa akivua samaki pembeni mwa mto Nile, akamvua nusu mtu nusu samaki,kiumbe huyu wa Nile aliitwa dagoni au Nimrod aliyerudi kuwa hai, na dagoni ni utambulisho wa Nimrodi ( yaani wa Babeli ya kale aliyeifufua dini ya Freemasons ) aliibuka majini kama nusu samaki nusu binadamu.
Wababeli wanaamini kwamba alama ya mungu aliye nusu binadamu nusu samaki ni tukio lililotokea kutoka Bahari ya Erythraean na kusimuliwa Babeli siku za mwanzo za historia yake.
Uwakilishi wa mungu-samaki huyu ulipatikana pia kwenye masanamu ya mji wa Ninawi,mungu dagoni wa wafilisti alikuwa pia na tabia sawa kama yule wa Babeli ( manners and a customs of the Bible ; by James Freeman).
Ibada ya dagoni pia iliathiri ulaji wa chakula kwa binadamu hapo kale, hii inaweza kuelezea siri ya kwa nini baadhi ya madhehebu wanakwepa kula samaki siku zote isipokuwa siku za ijumaa tu? kwa sababu wanatekeleza ibada za kale za kipagani za kumuabudu mungu dagoni ( The catholic Encyclopedia)
"Kama ilivyo kwa ibada za kuabudu kwake wote tunafahamu kutoka katika maandiko ya kale kwamba, kwa sababu za kidini Wasyria wengi walikataa kula samaki,tabia ambayo yeyote anaweza kuiunganisha na ibada za mungu samaki (The Catholic encyclopedia 1913 encyclopedia press,Inc.)
Hadithi za dagoni zinakwenda kale na kuelezea jinsi kundi la miungu walioshuka kutoka juu mbinguni na kuja kuwafundisha watu waabudu wa dagoni kuhusu unajimu,miungu hawa waliitwa samaki watu wakilinganishwa na pomboo watu, kwa uwezo wao wa kuvuta hewa kama binadamu na pia kujua kwamba dagoni alitumia alama za Ankh wa Misri kama alama ya uzima.
Siku hizo za kale kanisa lilichukua utamaduni huu wa Nimrod,kofia ya Papa, Joho lenye umbo la samaki kama yale ya mapadri wa ibada za samaki dagoni, kofia ya Papa pia imepambwa na alama za mungu saturn, Saturn inaitwa pia nyota ya Daudi ,au mhuri wa Solomoni ambao ni wa Babeli zamani kwa Nimrod ( pia ulitumiwa na kabila la dagoni) ambao pia Mungu aliulaani na kuuita nyota ya Moloch au Remphan,mungu ng'ombe ambaye Nimrod alimwabudu ,pia akawapeleka waisrael kuwa mateka wa Babeli sababu ya hili ,pia aliharibu hekalu la Solomoni.
Shetani wa kipagani dagoni, alikuwa ni mungu samaki, alikuwa ni mungu wa nafaka,kijana wake aliitwa Baali wa kwenye Biblia katika Agano la kale, Waebrania walijitolea divai ,ngano na mafuta kwa Mungu, lakini hasira ya Mungu ilikuwa juu yao kwa sababu waliabudu miungu yao ya uongo kama huyu Baali Mtoto wa Dagon.
"Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye aliyempa ngano, divai na mafuta , na kumuongezea pesa na dhahabu ,walivyomtumia kwaajili ya Baali " ( Hosea 2:8).
Sanamu la Baali la wafilisti ni la mtu mwenye ndevu nyingi na mwenye nguvu, tunaweza kuona picha za binadamu katika mawe huko kote Washington DC ,au wenye masikio ya ngano katika nywele zao, mafundisho ya siri yanaeleza kwamba Baali aliuawa na Mungu wa kifo na baadae aliamshwa.
Nabii Eliya aliwafanyia dhihaka waabudu Baali katika mlima Carmel ,1 Wafalme 18: 27 "ikawa wakati wa adhuhuri,Eliya akawafanyia dhihaka akasema mwiteni kwa sauti kuu,maana Mungu huyo ( Baali) au anasafiri, au labda amelala ,sharti aamshwe.
Sanamu lililoamshwa limewekwa katika mchanga pwani ya ya mto Potomac huko National Harbor in Prince Georges' County,Maryland.
Mwaka 2008 kampuni ya Peterson,wajenzi wa National Harbor walilinunua sanamu hilo na kulipeleka huko Washington DC kutoka Haines point kwenye eneo lake la sasa.