NA DIRAMAKINI
MWENYEKITI wa Ushirika wa Wachungaji wa Kipentekoste nchini, Askofu Pius Erasto Ikongo amesema, watumishi wa Mungu wote nchini wana dhamana kubwa ya kuiombea Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Askofu Ikongo ameyabainisha hayo kupitia taarifa aliyoitoa ikifafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imejipambanua katika picha ya maridhiano ya kisiasa, kijamii na imeonesha usikivu mkubwa.
"Watumisi wa Mungu wote tuna kazi ya kuiombea Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,maana Serikali hii imejipambanua katika picha ya maridhiano ya kisiasa na kijamii, na ni Serikali sikivu mno,"amefafanua Askofu Ikongo.
Pia, Askofu Ikongo amesema, watumishi hao wa dini wanapaswa kuliombea Jeshi la Polisi ambalo kwa sasa kupitia Mkuu wa jeshi hilo, IJP Camilius Wambura amekuja na mikakati thabiti ya kurejesha mahusiano mazuri kati ya polisi na raria.
"Ni kwa kutuletea polisi kata ambao wanafanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wa kata kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa. IJP Wambura amerejesha polisi jamii na pia amefungua milango ya kupokea maoni ya wananchi na kufanyia kazi kwa uwazi kabisa.
"Naomba watumishi wa Mungu tuendelee kuonesha ushirikiano wa karibu kwa Serikali, na endapo wakitokea watendaji wachache wanaomuangusha mama yetu Dkt. Samia zipo njia za kuwashughulikia.
"Hii nchi ni yetu hatutakiwi kuishi kwa hofu wala wasiwasi maana hatuna Taifa lingine tulilopewa na Mungu zaidi ya Tanzania,"amefafanua Askofu Ikongo.