NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya uteuzi wa kukamilisha safu ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Sophia Edward Mjema.
Kwa sasa, safu ya wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) imekamilika baada ya kutangazwa.
Ni baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimefanyika leo Januari 14, 2023 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akitoa taarifa ya kikao hicho, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema, Kamati Kuu ya chama iliketi na vikao vyote vilihitimishwa na Halmashauri Kuu chini ya mwenyekiti wake.
“Pamoja na mambo mengine ya kupokea na kufanyia kazi taarifa mbalimbali za chama, kikao kimeteua safu mpya za wajumbe wa NEC na kuidhinisha sekretarieti. Wajumbe sita wamechaguliwa ambapo watatu wanatoka Tanzania Bara na watatu Zanzibar ili kukamilisha wajumbe wa kamati kuu kufika 24, hawa saba kwa mujibu wa katiba wamechaguliwa na safu,” amesema Shaka.
Shaka amesema mwaka 2022, chama hicho kilikuwa na uchaguzi wa chama ngazi ya shina mpaka taifa na baada ya kumaliza Hamalshauri kuu ya Taifa imefanya uteuzi wa kukamikisha safu ya wajumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi.
Amewataja wajumbe kutoka Bara kuwa ni pamoja na Mizengo Pinda (Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Hassan Wakasuvi (Mwenyekiti CCM Tabora), Halima Mamuya ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Shaka, kwa upande wa Zanzibar amemtaja Mohamed Abood Mohamed,Mhandisi Nasri Ally na Leyla Burhan Ngozi akisisitiza kuwa kila upande nafasi mbili zilikuwa za wanaume na nafasi mbili wanawake.
Pia amesema kikao hicho kimeithibitisha Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya Taifa na kutaja orodha ya wajumbe waliochaguliwa.
Amesema, nafasi ya Katibu Mkuu ameendelea Daniel Chongolo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Annamringi Macha, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mohemed Said Dimwa.
Shaka amesema nafasi yake ya Katibu Itikadi na Uenezi imechukuliwa na Sophia Edward Mjema (Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dkt.Frank Hawasi, Katibu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Mbarouk Nassoro na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu.