Wafuasi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam wameendelea kuonesha upendo wa kipekee kwa Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ambaye pia ni mwekezaji mkubwa katika klabu hiyo.
Kwa nyakati tofauti wafuasi hao wamekuwa bega kwa bega na mwekezaji huyo ambaye baada ya kupata nafasi ya kuwekeza hivi karibuni aliifanikisha klabu hiyo kustawi zaidi ndani na nje ya nchi.
Biashara kubwa ambayo inafanyika katika klabu hiyo ambayo pia ina vitega uchumi kadhaa ni kutumia nembo ili kutengeneza faida, mauzo ya jezi, skafu, haki za majina za Simba pamoja na bidhaa nyingine zinazoweza kutengenezwa na klabu hiyo.
Pia kushirikiana na wadhamini wakubwa ambao wanaweza kutoa fedha, huku pia akipandisha thamani ya wachezaji wa timu hiyo ili iweze kuvuta mashabiki wengi zaidi uwanjani ikiwemo kuuza wachezaji ndani na nje.