Haikubaliki, chukueni hatua-Waziri Kairuki

NA ANGELA MSIMBIRA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (OR-TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amekerwa na kasi ndogo ya uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, elimu ya awali na elimu ya msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro mkoani Kagera.

Kairuki ameyasema hayo Januari, 18, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa elimu na uwekaji wa mpango kazi wa utekelezaji kwa mwaka kilichofanyika mkoani Kagera.

Amesema, takwimu za uandikishaji wa elimu ya awali zinaonesha Mkoa wa Kagera una wastani wa asilimia 82, lakini kuna baadhi ya wilaya ziko nyuma hali inayoonyesha kuwa bado elimu inahitajika kutolewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwaandikisha watoto shuleni.

Kairuki amesema katika eneo hilo Halmashauri ya Wilaya ya Biharamuro ina asilmia 56, Manispaa ya Bukoba asilimia 75, Ngara asilimia 78, Muleba asilimia 81, Halmashauri ya Wilaya Bukoba 107, Karagwe asilimia 100, Kyerwa asilimia 86 na Missenyi asilimia 97.

Amesema kuwa, kwa upande wa uandikishaji wa darasa la kwanza Mkoa wa Kagera una wastani wa asilimia 89 ambapo Biharamuro imekuwa ya mwisho kwa kuandikisha wanafunzi kwa asilimia 76, Bukoba 101, Manispaa ya Bukoma 96, Karagwe 101, Kyerwa 86, Missenyi 102, Muleba 83 na Ngara asilimia 88.

Kairuki amesema, kwa uandikishaji wa kidato cha kwanza bado mkoa umefikia asilimi 46 huku Biharamuro imekuwa ya mwisho kwa kuandikisha wanafunzi kwa asilimia 16, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba asilimia 62, Missenyi asilimia 20, Karagwe asilimia 50, Muleba asilimia 63, Ngara asilimia 52, Kyerwa 50 na Bukoba asilimia 43.

Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanaweka makakati wa kuongeza kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi ndani ya muda mfupi ili watoto waandikishwe bila vikwazo.

Kairuki amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanaweka mkakati wa kuwashirikisha viongozi wa Dini,viongozi mashuhuri, viongozi wa kimila na watendaji katika ngazi mbalimbali za Serikali kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhimiza jamii kuhusu umuhimu wa kuwaandikisha wanafunzi shuleni.

Amesema, kunakuwa na madhara makubwa pale mtoto anapochelewa kuandikishwa elimu ya awali kwa kuwa inampa mwalimu wakati mgumu kumpima mtoto huyo kwa kuwa tayari anakuta watoto wengine wameanza kujifunza

"Serikali itakapoanza kufanya tadhmini ya kuangalia wanafunzi wamefikia kiwango gani cha uelewa lazima kutatokea madaraja baina ya wanafunzi na kuwa naombwe kubwa,”amesema.

Pia amewataka kuweka msukumo katika uandikishaji wa wananafunzi wa elimu ya awali na iwekwe kuwa ni ajenda namba moja kwa kila kiongozi ndani ya Halmashauri lengo likiwa ni kufikia malengo ya asilimia 100.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news