Huyu ndiye mchungaji anayezua maswali kwa kuvaa viatu virefu vya kike wakati akihubiri

NA DIRAMAKINI

MCHUNGAJI Ben kutoka nchini Togo huko Magharibi mwa Afrika ambaye alidai kuwa Mungu alimtokea na kuamuru avae viatu vyenye visigino virefu kwa ajili ya huduma ameendelea kuibua maswali mengi katika mitandao ya kijamii huku yakikosa majibu ya moja kwa moja.
Ben katika siku za karibuni alizua tafrani barani Afrika baada ya picha zake kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii huku akihubiri neno la mungu akiwa amevalia viatu virefu.

Kulingana na ‘mchungaji wa viatu virefu’ anavyofahamika, mungu alimwagiza aanze kuvaa hivyo baada ya miaka mingi ya kusali ili apone maumivu ya mwili yasiyovumilika ambayo yalikuwa yanamkabili.
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba kwa mujibu wa mtu huyo anayejiita wa mungu, alikuwa akivaa viatu vya kiume na kupata maumivu ya mwili na magonjwa mengine mengi, lakini tangu alipotii mwongozo wa mungu na kubadili viatu virefu, maumivu yake yalipungua.

"Sivai nguo za kike kama watu walivyosema kwenye mitandao ya kijamii, lakini ninavaa viatu vya kila aina, kulingana na muongozo niliopokea kwa mungu,"alikariria mchungaji Ben.
Siku za karibuni, baadhi ya watu ambao wanajivika majoho ya utumishi wa Mungu wamekuwa wakitenda mambo ya hovyo hovyo ambayo wakati mwingine visa hivyo vimekuwa vikitoa maswali yanayokosa majibu ya moja kwa moja.
Mathalani, mwaka juzi, mhubiri mmoja alipamba vichwa vya habari kwa kuwanyunyizia waumini dawa ya kuua wadudu akidai itawaponya ukimwi, huku kisa kingine kikimuhusu mchungaji wa kiume kutoka Afrika Magharibi akiwabusu waumini wa kike, akisema kwamba bwana ndiye aliyemwelekeza kufanya hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news