IJP Wambura atoa orodha ya majina ya vijana walioomba kuajiriwa Jeshi la Polisi, soma hapa

NA GODFREY NNKO

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camilius Wambura amewatangazia vijana walioomba kuajiriwa na Jeshi la Polisi usaili wao utafanyika kuanzia Januari 23, 2023 hadi Februari 3, 2023 nchini kote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 17, 2023 na IJP Wambura, waombaji wenye elimu ya kidato cha nne waliowasilisha maombi yao kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa usaili wao utafanyika kwenye mikoa waliyowasilisha maombi yao.

Aidha, waombaji wa Zanzibar wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada usaili wao utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na waombaji wenye elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kwenye mikoa waliyowasilisha maombi yao.

"Waombaji wa Tanzania Bara wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada ambao walituma maombi yao kwa njia ya mtandao, usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika Vikosi vya Polisi vilivyoainishwa kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.

"Aidha usaili huo utafanyika kwa makundi mawili (2), kundi la kwanza litaanza Januari 23,2023 hadi Januari 27,2023 na kundi la pili litaanza Januari 30, 2023 hadi Februari 3,2023.

"Kila mmoja atatakiwa kufika na vyeti halisi vya taaluma (academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya NIDA na cheti cha JKT au Barua ya Uthibitisho toka kwa Mkuu wa Kambi (Kwa vijana walio kwenye makambi ya JKT/JKU),"amefafanua IJP Wambura kupitia taarifa hiyo.Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili jijini Dar es salaam hii hapa chini;
Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili majina zaidi bofya hapa chini


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news