NA DIRAMAKINI
JESHI la Polisi Tanzania limesema, hali ya ulinzi na usalama wa nchi ni shwari, kwani matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa.
Hayo yamebainishwa leo Januari 26, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania makao makuu jijini Dodoma, SACP David A. Misime.