KASULU KUUKARIBISHA MWAKA KWA BONANZA

NA RESPICE SWETU

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma inatarajia kufanya Bonanza la Watumishi litakalohusisha michezo mbalimbali.

Akitoa taarifa ya bonanza hilo, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Charles Mvuyekule amesema kuwa, Bonanza hilo litakalofanyika Januari 7, 2023 litahusisha michezo ya soka kwa wanaume, mpira wa pete, kuvuta kamba, kuruka, riadha na mbio.

Ameongeza kuwa, maandalizi ya Bonanza hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Kasulu, yanaendelea vizuri na kuwaomba watumishi wa halmashauri hiyo kujiandaa kwa kufanya mazoezi yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye bonanza hilo.

"Kupitia bonanza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Joseph Kashushura atazungumza na watumishi,"amesema.

Bonanza hilo litakaloambatana na chakula cha usiku, litakuwa la pili kufanyika katika historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kufuatia lililofanyika mwaka 2021.

Pamoja na kuitumia michezo kudumisha mshikamano miongoni mwa watumishi wa halmashauri hiyo, bonanza hilo pia litakuwa ni la kuukaribisha mwaka wa 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news